Friday, February 14, 2014

THESUPERSTARSTZ:::ELEWA UNAPOMPIGA MWANAMKE PICHA ZA UCHI UNAMDHALILISHA MAMA NA DADA ZAKO JIULIZE IKITOKEA KWA MAMA YAKO JE?


Ni kile kinachoonekana kutofautiana kati yake na mpenzi wake hadi kupelekea jamaa kuzianika picha za mpenzi wake hadharani eti kwa malengo ya kumkomoa kimwanana huyu aliyeachana nae katika hali ya ugomvi.
 
Cha kijiuliza hapa ni kuwa wewe mwanaume unayefanya hivi utajisikiaje siku dada yako au mama yako akianikwa uchi na wanaume wenzio.
 
Amini baadhi yetu tunafurahiya na kuwalaumu wanawake kwakupigwa picha hizo ila mimi ninawazo tofauti nadhani hata wanaume wakiacha kuwapiga picha hizo jamii yetu itakuwa salama lakini kama lawama kila siku zikienda kwa wanawake basi jua hakuna litakalofanyika kila siku tutegemee kuona tupu za mama zetu na dada zetu zikianikwa kama maembe au nyanya sokoni.
Inaniuma sana kuona jamii imefikia hatua ya kushangilia haya na kuayaona ya kawaida ila tunapoteza utu wa mwanamke ambaye ni mama yetu na dada zetu na watoto wetu kwa ujumla.
 
Ombi la thesuperstarstz kwenu ni kwamba tupo chini yenu tunaomba ifike wakati tuwe na uchungu na tuone aibu kama ilivyo wewe kuona tupu ya mama yako pia wanaume tuache kuwadhalilisha wanawake kwakuwapiga picha hizo lakini pia mama na dada zetu tuwe makini tusilewe mapenzi kiasi hicho hadi kukubali kila tunachoambiwa maana utaharibu safari ya maisha yako kwa dowa la picha za uchi kila utakalolitaka katika jamii iwe uongozi wa kawaida hata maisha ya kawaida watu watatumia picha zako kama fimbo.
HONGERA SANA WW MWANAMKE UNAYEJITAMBUA,NA ASANTE WEWE MWANAUME UNAYESIMAMA KAMA BABA NA KUTOKUFANYA UJINGA WA KUMDHALILISHA MAMA YAKO AU DADA ZAKO.


3 comments:

  1. Duh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. Jinga sana wewe. sasa kwa nini wewe unadhalilisha still kwa kupost hizi picha?

    ReplyDelete
  3. IRENE ACHA UNAFKIIIIIIIII WHAT ABOUT YOUR OWN NUDE PICS KIBAO MTANDAONI???

    ReplyDelete