Saturday, February 15, 2014

TV 1 KITUO KIPYA CHA BURUDANI '' CHAANZISHWA NCHINI, VANESSA MDEE GEORGE TYSON WAHUSIKA

Vanessa Mdee

Vanessa Mdee anazidi kung'ara katika tasnia ya utangazaji baada ya kituo kipya nchini cha TV1 kumchukua kufanya nae kazi kama mtangazaji wa kipindi cha "The One Show" kitakachohusika na entertaiment kama vile filamu, muziki, fashion na mengineyo. TV1 ni kituo kipya cha burudani nchini kinachomilikiwa na kampuni ya Modern Times ya nchini Sweeden. Kwa mujibu wa Bongo5 George Tyson aliyekuwa mume wa Monalisa ndiye director wa vipindi katika kituo hicho chenye office zake Mikocheni jijini Dar es salaam. The One Show itaanza kurushwa hewani mapema mwezi ujao na kwasasa tayari vipindi kadhaa vimeshashutiwa.

Kituo hicho cha Tv kitakuwa kikihusika na masuala ya burudani kwa kiasi kikubwa kuanzia filamu, muziki, fashion na mambo mengine kutoka Tanzania na ya kimataifa. Hii inaonyesha kuwa sanaa na wasanii wa Tanzania wanakubalika ndani na nje ya nchi ndiyo maana wawekezaji wa kigeni kama Modern Times Group wameamua kuwekeza katika sector ya burudani nchini.

TV1 tayari inaonekana katika ving'amuzi vya Startimes na inatarajiwa kuleta ushindani katika sekta ya burudani nchini kutoka kwa vituo vingine maarufu kama vile EATV, Channel Ten, ITV, Clouds Tv, DTV, Star Tv na vinginevyo.

Logo ya TV1
George Tyson director wa vipindi TV1...............

No comments:

Post a Comment