Sunday, March 30, 2014

FREEDOM FIGHTER TAJIRI MTOTO MWENYE MALENGO YA KUZIFIKISHA FILAMU ZA BONGO HOLLWOOD

Hapa freedom Fighter Tajiri Mtoto akiwa pozi katika moja ya gari lake la kutembelea 
Tunapozungumzia filamu tanzania ni tasinia inayokuwa kwa kasi ya ajabu na kujikuta inakubalika kwa mashabiki na hata kwa wawekezaji wa fani hiyo ambayo imekuwa kimbilio la ajira hapa nchini.

Akipiga stori na mtandao huu wa thesuperstarstz mapema hii leo ofisini kwake jijini mwanza mwekezaji na msanii wa filamu nchini anayekuja kwa kasi ya ajabu na kutishia nafasi za mastar wa filamu nchini Freedom Fighter mwenye makazi yake jijini mwanza amesema kuwa yeye amejipanga kuhakikisha sanaa hii inakuwa kwasababu ni kitu alichokuwa amedhamiria kukifanya muda mrefu...Kiukweli sanaa ipo katika damu na ndio maana unaona nimewafadhili mastar wengi wa filamu na wanamuziki pia lengo likiwa ni kuinua sanaa yetu alisema freedom.
Hapa freedom fighter akiwa  katika pozi
Mwandishi wetu alipata bahati ya kukutana na wasanii kadhaa wakiwemo mastar ambao wapo mwanza kwa ajili ya kufanya usaili wawasanii wa filamu wakiwa ofisini kwa mwanaharakati huyo na kumuelezea jamaa kama nguzo muhimu sana katika sanaa hapa nnchini.
 
Hapa freedom fighter akiwa na Vicent Kigosi Ray

Mbali na kusaidia watu hivi sasa freedom ameanzisha kampuni yake ya maswala ya filamu inayotumia nembo ya freedom fighter filim company ikiwa tayari ipo katika maandalizi ya filamu zake mbili kwa mpigoambapo inatarajia kumshusha Irene Uwoya na hemedi katika filamu moja na nyingine watakayomshirikisha king majuto na hemed kwa upande wake freedom anasema amejipanga kisanii sana na atahakikisha anaifikisha sanaa mbali kama mungu akimpa uhai...
Hapa freedom wa mbele mwenye shati la mistari akiwa na msanii wa filamu nchini Wastara Juma wa katikati na wasanii wengine
Freedom anaendelea kuweka wazi mikakati yake kuwa hivi majuzi alikamilisha mambo muhimu ya kuifikisha sanaa ya bongo nnje ya nnchi..Kifupi nimeanza mikakati ya kuinua sanaa yetu kwa njiaa nyingine tofauti na ile ya kutoa pesa kuwapa wasanii wakatengeneze filamu au kurecodi nyimbo zao nimeanzisha mkakati utakao wawezesha wasanii watanzania kufika hollwood kimasomo ili kuijua zaidi sanaa  pia kwa upande wa afrika nimeanzisha mkakati wa kuwaleta wasanii wa nnje na kuwachukuwa wa hapa kuwapeleka south africa,ghana,nigeria na nnchi nyingine alisema msanii huyo mwenye wingi wa huruma kwa sanaa ya tanzania.

Nnje ya sanaa freedom ni mfanya biashara maarufu ndani na nnje ya nchi thesuperstarstz inamuomba mdau huyu muhimu kutokataa tamaa  na kumtaka aendelee kusaidia sanaa kwa ujumla ili kuikuza sanaa yetu hapa nchini

No comments:

Post a Comment