Monday, March 31, 2014

MR BLUE.....MUZIKI WETU HAUTOKUWA KAMA MASTAR HAWATAWAJALI MA UNDERGROUND

Mr Blue wa pili kutoka kushoto akiwa na wasanii wenzake
Msanii mkali wa bongo fleva na mwenye heshima kubwa katika mziki wa bongo mr blue ambaye ni baba wa mtoto mmoja ameamua kufanya jambo la kuigwa na waanii wengine ili kukuza muziki wa tanzania.

Akipiga story mbili tatu maeneo ya tabata anapoishi msanii huyu ameeleza hisia zake kwa ma underground wa muziki huo huku akisema ni wazi muziki wetu unakosa muelekeo kwa kutokuthamini wanamuziki wachanga..Unajua mkubwa wanamuziki wanajiangalia wao tu na ndio maana muziki wao ukiisha unaisha vibaya kwa sababu hakuna walichokiwekeza kwa wasanii wachanga nadhani utakubaliana na mimi kuwa nimekuwa msaada mkubwa kwasanii wachanga toka mwanzo jambo ambalo linanifanya nione furaha kila nionapo nyota niliowapa shavu au walionipa shavu katika ngoma zao wakishaini leo alisema msanii huyo.
Kiukweli blue ni kati ya wasanii wachache wanaokubali kutoa kampani kwa muziki huu haswa kwa wasanii wachanga alisikika akisema msanii mmoja underground toka mwanza,ambapo maneno hayo pia yaliungwa mkono na msanii Ivory wa mwanza na mwanadada najma mtanzania anaishi na kufanya muziki nchini uingereza.

Mbali na hao thesupestarstz ilifanikiwa kuongea na king wa R&b Steve R&b na kuweka wazi kuwa blue ni nguzo muhimu sana kwa wasanii wachanga kwani ni mwepesi kusikiliza na kukupa ushauri juu ya muziki unaotaka kuufanya na kama ukimuhitaji katika ngoma yako basi hasiti kukusaidia alisema steve.

Baada ya dodosa dodosa hizi thesuperstarstz ilimvutia waya blue kumpongeza lakini pia kupata mawili matatu nae alikuwa na haya....Kiukweli hakuna aliyeinuka kitandani na kuwa star wote tumepitia hatu za kuwa wasanii wachanga ndio tukafika hapa baada ya mashabiki kutukubali sasa sioni sababu ya kutokuwasaidia hawa wanaotaka kuwa wasanii kwakuwa hujui kapangiwa nini alisema blue.

Mr Blue
Muandishi wa thesup[erstarstz alitaka kujua ni wasanii wangapi aliowasaidia hadi leo ambapo blue alidai ni wengi sana na pia sio vizuri kuwataja kama wao hawajaona umuhimu wakufanya hivyo....Tukianza kuhesabu kaka tutakesha kifupi ni wengi sana na wengine tumewasaidia hadi kurekebisha ngoma zao yaani kuwaandioa na kuwapa sauti na leo ni mastar wakubwa tu ila sio poa kumtaja mtyu kama yeye hajaona umuhimu waakukutaja ama kukushukuru  ila moyoni anajua kuwa mangapi nimemsaidia  na sintoacha kuwasaidia wasanii wenzangu pale nitakapoweza alimaliza blue

Msanii huyu mkali wa mashairi na floo za uhakika aliendelea kutiririka na kusema kuwa kwa upande wake hachagui msanii wa kufanya nae kazi na kuongeza kuwa yeyote atafanya nae ilimradi ngoma iwe kali na i muinue msanii husika.

No comments:

Post a Comment