Monday, March 03, 2014

NISHA ADONDOSHA MACHOZI HADHARANI KISA MASHABIKI NA UNDEGROUND SOMA KILICHOMKUTALady Bosi wa Nisha Films Production Salma Jabu(NISHA)

Mwanadada star ambaye pia ni produser ndani ya kiwanda cha filamu bongo Salma jabu maarufu kwa jina la nisha leo amefunguka na kuongea ya moyoni kuhusu mashabiki wake.Akizungumza na mwanahabari wa thesuperstarstz nisha amesema anayo kila aina ya sababu ya kuwashukuru mashabiki wake ndani na nnje ya tanzani kwa wamekuwa na mchango mkubwa sana na kila akiwakumbuka huwa haoni cha kuwalipa mashabiki wake.


Nisha ni msanii mwenye historia ndefu na ni kati ya wasanii waliosota na kuteswa kunyanyasika sana katika tasnia hii hadi alipofanikiwa kujulikana kwa mashabiki zake na kumkubali kazi zake,huwezi amini kasasa gumzo inaongoza sokoni na imewabamba watu sana kiukweli imekuwa gumzo mjini kama ilivyo jina lake,kwasasa nisha kwa sasa anamiliki saloon ya kisasa na mali kadhaa ikiwemo gari lake la kifahari .
Mwanadada huyo mrembo na anayekimbiza sokoni kwa sasa amezidi kwenda mbali zaidi huku akidondosha machozi kwa kusema haamini mashabiki zake wanachomfanyia..Kiukweli nashindwa kuwa na kauli ya asante kwa wadau na mashabiki zangu kwa jinsi wanavyoni suppot mara niingizapo kazi sokoni,kuikweli nasema mbele ya mungu kuwa gumzo inafanya vyema sana na hii ni kwa sababu najitaidi kuwapa mashabiki kile wanachokipenda alisema nisha.
Akizidi kwenda mbali zaidi nisha huku machozi yakimtoka na kumpa kazi mwandishi wetu kumtuliza alisema kuwa hakuna kitu kinachomuumiza maishani mwake kama wasanii chipukizi ambao wanahangaika kutoka na kunyanyasika kama alivyonyanyaswa yeye,ila sasa anaamii mungu amemteuwa kwa ajili ya kuwasaidia,pia nisha amewataka mashabiki wake  kutokuwa na mawazo kuwa nisha atakuja kubadilika...Kaka nataka mashabiki zangu wajue nisha yule yule toka Enzi ya pusi na paku tikisa na hata gumzo ama kwa hakika najali sana mashabiki zangu wanachotaka kutoka kwangu aliongeza nisha huku akijifuta machozi.

Mwisho nisha amewashukuru crew yake na kusema kuwa wao ni muhimu sana kwa nisha na wanafanya kazi kubwa sana kuhakikisha nisha anakuwa nisha...iukweli naishukuru sana crew yangu Cameraman,Ligth,sound,edta,mtu wa mavazi makeup,na wote wanaonifanya nisha niwe hapa nilipo alimaza nisha.
Thesuperstarstz inamtakia nisha mafanikio na maisha marefu ili aendelee kuiwakilisha vyema tasnia ya filamu Tanzania

No comments:

Post a Comment