Sunday, March 30, 2014

WEMA SEPETU APOKEA SMS ZA VITISHO ILI AMUACHE DIAMOND RAFIKI WA PENNY AONGEA NA THESUPERSTARSTZ

Wema sepetu akiwa na Diamond platnum
Msanii wa bongo movie ambae pia ni bosi lady na mwanamke anayeongoza kwakufuatiliwa na vyombo vya habari nchini kutokana na swaga zake maadamu wema sepetu leo ametoa ya mwaka kufuatia sms anazopokea zikimtaka aachane na kipenzi chake diamond kwa kisingizio cha kuiba bwana wa mtu.
Wema sepetu katika pozi
Wema ambaye pia ni msanii wa filamu na anaetamba sokoni na filamu ya Madamu amejikuta katika wakati mgumu mara baada ya kurudiana na Diamond  mwanamziki ambaye yupo juu kwasasa na kujikuta akipata sms zisizo na idadi zikimtaka achane na mwanamuziki huyo kwakuwa analazimisha mapenzi kwa mkali huyo wa my number one.

Diamond akiwa na wema sepetu
Chanzo cha habari hii ambacho ni rafiki wa karibu wa wema sepetu kimeipasha thesuperstarstz kuwa wema amekuwa akipokea sms za vitisho zikimuambia kuwa yeye ni mwizi wawaume za watu huku zikimtaka aachane na diamond haraka iwezekanavyo..Ni ukweli kabisa hata wema alipotoka Air port kumsindikiza Mchumba wake alipokea sms ikisema Achana na mchumba wangu maana na jua hakuna mapenzi hapo zaidi ya kulazimisha tu kilisema chanzo hicho bila kupepesa macho kwa masharti ya kutokutajwa jina
Diamond akiwa na penny enzi zao
Mtandao huu uliendelea kumdadisi mtoa stori na kusema yeye anahisi hizo sms zinatoka kwa Penny ambaye alikuwa mchumba wa Msanii huyo mkali katika mziki kwa sasa na kusema Penny amekuwa akiumia sana kuona wema na diamond wapo pamoja jambo ambalo sio sahihi kwakuwa penny alimkuta diamond akiwa na wema kama wapenzi sasa haelewi kinachomuuma peny kwakuwa Diamond amerudi nyumbani kwake kililonga chanzo hicho makini ambacho kinaonekana kutokumpenda penny.
Penny katika pozi
Thesuperstarstz ili kubalansi ukweli wa habari hii ilimuendea hewani penny ila hakupokea simu nikabidi kumpigia rafiki yake ambaye nae alijibu kifupi kuwa hayo hayamuhusu ila anachojua yeye penny yupo bize na mambo yake so  wema angemuacha maana penny hana time ya kujadili ujinga.

No comments:

Post a Comment