Monday, May 26, 2014

JOTI NI NOMA AFANYA MAKUBWA NDANI YA SANDUKU LA BABU

Lucas Mhuvile 
Joti mwigizaji wa filamu na vichekesho Swahiliwood
MSANII wa Komedi Bongo Lucas Mhuvile ‘Joti’ ametengeneza filamu inayokwenda kwa jina la Sanduku la Babu, msanii huyo anajivunia aina ya mfumo aliotumia katika kuandaa sinema hiyo kwa kuirekodi na kushiriki katika nafasi zote pekee yake na kuifanya kuwa filamu sawa na iliyoshirikisha wasanii wengi.Filamu hiyo ambayo inaonekana ni ya maajabu ni kutokana na Teknolojia iliyotumika kwa nafasi zote kuchezwa na mhusika mmoja, Joti amecheza katika sinema ya Sanduku la Babu kucheza nafasi ya Babu wa Sumbawanga, Bi. Kiboga, Amijee, na kuwashirikisha kidogo wasanii chipukizi.

Lucas Mhuvile
Joti akiwaonyesha waandishi wa habari Posters ya Filamu yake ya Sanduku la Babu
Lucas Mhuvile
Joti akiwa katika pozi
Lucas Mhuvile
Bi. Kiboga akiwa katika pozi zake ndani ya filamu ya Sanduku la Babu
Lucas Mhuvile
Joti katika Pozi la kusaka Pesa
“Nilikuwa nikifikiria sana kuhusu kuingia katika tasnia ya filamu kwani nilitaka kujua baada ya kutengeneza kazi yangu nitaipeleka wapi? Lakini baada ya kukutana na Proin Promotion nilibaini kuwa hawa wanaweza kufikisha kazi yangu ninapotaka ifike, hivyo ninaiingiza sokoni tarehe 26. May. 2014,”anasema Joti.
Naye msemaji wa kampuni ya Proin Promotion Mr. Evance amesema kuwa kampuni imejipanga kuhakikisha kazi ya Sanduku la Babu inamfikia kila mtu kwani msanii huyo ni kipenzi cha wapenda filamu na vichekesho nchini, kampuni imejipanga kuwafikishia walaji kwa wakati muafaka.
Joti anasema kuwa kazi hiyo ameiandaa kwa muda wa miaka miwili, kulingana na Teknolojia iliyotumika kwani kila mara ilimpasa baada ya kutengeneza na kuangaliwa na watalaamu kisha kumweleza abadilishe matukio kitu kilichomfanya atumie muda mrefu.
Msanii huyu ambaye anatoka katika kundi mahiri la Orijino Komedi, linaloundwa na wasanii kama Masanja Mkandamizaji, Mac Reagan Kipara, Mpoki Joti na Wakuvanga, pamoja na kutoka na sinema ya Sanduku la Babu bado yupo katika kundi hiyo ni sehemu ya kujiongezea kipato.

No comments:

Post a Comment