Monday, June 02, 2014

MSIBA ..ZITTO KABWE AMPOTEZA MAMA YAKE MZAZI


Bi Shida Salum, mama yake Zitto Kabwe katika msiba wa Mzee Makani.

Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, mchana huu amefiwa na mama yake mzazi aliyeugua kwa muda mrefu.

Bi Shida Salum, amefariki katika hospitali ya AMI jijini Dar Es Salaam ambako amekuwa akitibiwa kwa zaidi ya wiki mbili.
Awali Bi Shida alikuwa amepelekwa India kwa ajili ya matibabu kabla ya kurejeshwa nchini.
Zitto ni mbunge kijana kutoka CHADEMA, ambaye amepata umaarufu mkubwa kutokana na uhodari wake wa kujenga hoja.
Mama yake wakati wa uhai alikuwa mshiriki katika maswala ya kisiasa, ambapo alikuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA.
Thesuperstarstz tunatoa pole kwa Zitto Kabwe, familia na wote walioguswa na msiba huu.
Tutawaletea habari zaidi zitakavyopatikana.

No comments:

Post a Comment