Friday, October 24, 2014

DIAMOND SIFIKIRII KUWA NA BIFU NA MSANII YOYOTE NAANGALIA KAZI ZANGU,MENEJA WAKE APIGWA NA MSHANGAO


Ali Kiba Na Diamond Wasanii wenye mashabiki wengi nchin tanzania
Mwanamuziki wa kizazi kipya Nassibu Abdul ama Diamond amesema anashangazwa na habari za uvumi ambazo yeye haelew zinatoka wapi juu ya bifu,inayoenezwa kati yake na msanii mwenzie Ali kiba. Msanii huyo ameongea hayo na mwandish wa thesuperstarstz huku akionyesha wazi kukerwa na hali ile.

Akizungumza kwa uchungu nyumbani kwake sinza jijini Daresalam Diamond amesema kamwe hajawahi kufikiria wala kuhisi kama atakuja kuwa na bifu na Ali kiba au msanii mwingine yeyote kwani yeye na Ali hawajajuana katika muziki bali wamejuana kitambo kabla ya muziki hivyo wanaheshimianasana
Haya kaka kweli mmetoka mbali hapa Ali Kiba na Diamond
Msanii huyo amesema kuwa yeye ana amini kama Ali Kiba alihisi kuna tatizo kati yao basi Angemfuata au angempigia simu kumuuliza kwani uwezo huo kiba anao na ananimudu vizuri so sidhan kama kungekuwa na tatizo lolote la yeye kuniambia alisema Diamond.
Huu ni uthibitisho kuwa watu hawa wametoka mbali sana hapa Kiba/Diamond/na Marlow enzi hizo
Akizungumzia kilichotokea juzi katika Serengeti Fiesta Msanii huyo amesema yeye ana amini kuzomewa ni jambo la kawaida kabisa kwa msanii wa afrika na hii inatokana na fitina ambazo unafanyiwa na wapinzani wako lengo likiwa ni kukuangusha kwanamna moja au nyingine...Kwangu haikuwa kitu cha ajabu sana kwa lile tukio maana kwa msanii wa africa kuzomewa ni kitu cha kawaida maana hatuna utamaduni wakupenda cha kwetu lakini pia unaweza kuzomewa na kundi la watu flani ambao kwa kelele zao zikawafanya wengine kuzomea hata kama walikuwa hawana nia hiyo kwa hiyo ile ni changamoto na sintomlaumu mtu yeyote cha msingi bado nitaungalia mziki wangu kwa mbele zaidi ili siku moja watu wataona na kujua kwanini nilizomewa na mbinu ilifanywa akina nani na kwa lengo gani,kikubwa mimi nawaomba mashabiki zangu kuendelea kuniamini na kuwa wavumilivu wasije kujenga bifu na mtu yeyote maana huu ni muziki na sote tunasaka riziki? alimaliza msanii huyo mkubwa mwenye tuzo nyingi ndani na nnje ya tanzania.
Diamond akiwa na meneja wake anaitwa Babi Tale
Mdakuzi wako wa thesuperstarstz alipata bahat ya kuzungumza na Meneja wa Diamond anayejulikana kkwa jina la Babu Tale ambae kwanza alianza kwa kucheka kisha akasema Mkubwa sisi tunataka kazi na sio maneno kiukweli sisi hatupo tayari kuliongelea jambo lile kwakuwa tuna mambo mengi ya kufanya na kifupi nawashukuru mashabiki wa kweli wa Diamond kuona umuhimu wakuandika katika mitandao kile kilichotokea pale mimi nadhani inatosha sisi wacha tufanye kazi mkubwa maana kuna mengi yanakuja soon alisema Tale

Pia meneja huyo alitumia nafasi hii kuwaomba mashabiki wa Diamond haswa katika nchi hii ya tanzania kuwa tujitaidi kuwapenda wasanii wetu na kuwa suppot kama tunataka kuifikisha sanaa yetu mbali maana kumzomea msanii wako wa ndani unataka nnje ya nyumbani wamfanyeje kama sio kupiga hata chupa alisema meneja huyo na kuongeza kuwa kwasasa tuige mfano nnchi kama Nigeria ambayo ina wasanii chungu nzima wa music na filamu ambao wanavuma kimataifa na hapo tunaijua nageria kwa haraka kila tukiona filamu au nyimbo zao lazima uitaje Nigeria alimaliza Tale.
Mwandishi wetu alitaka kujua kama meneja huyo anaijua bifu ya Diamond na Kiba chanzo nini nae alikuwa na haya ya kusema,,,,Mimi toka nimemjua Ali kiba na Diamond sijawahi kuona wao kama wakiwa na bifu ila nimewahi soma au kusikia katika media mbali mbali zikielezea bifu hiyo na hata sisi tulikuwa tunashangaa lakini kwasasa tunagundua ukimya wetu ndio umetufikisha hapa kumbe tungekemea kipindi kile au kiba angekemea wala kusingejengeka haya ya leo kifupi hakuna Bifu kati ya Diamond na Ali kiba na kama Kiba anahisi kuna tatizo aweke wazi na hata yeye ukimuhoji atakuambia haelewi nini tatizo na hana bifu yoyote na mwinzie kwahiyo mashabiki wakati mwingine sio kila habari unayosoma au kuisikia ipo sahihi nyingine zipo tu kwa ajili ya promo flani alisema meneja huyo

Kwa maon yetu tunaona hakuna anyemfikia mwenzia kwani Diamond hawezi kuwa Ali kiba Na Ali kiba hawezi kuwa Diamond tujitaidi kuwapenda wasanii wetu wote ili watufikishie mbali sanaa yetu kwa vizazi vijavyo

Kwa habari za wasanii matukio na michezo Usikose kutembelea mtandao huu click hapa www.thesuperstarstz.blogspot.com

No comments:

Post a Comment