Thursday, October 23, 2014

SELEMBE TOKO STAR WA MOVIE ZA KISWAHILI BARANI ULAYA AIVAMIA GENNEVA USWIZI


Selembe Toko katika pozi
Msanii wa filamu za kiswahili ambaye anatamba hivi sasa katika angala la filamu za kiswahili huko barani ulaya na viunga vyake anayejuikana kwa jina la Selembe Toko mwenye makazi yake nchini Denmark leo ameongea na thesuperstarstz akiwa nchini Genneva Uswizi ambako yuko huko kimapumziko.
Selembe akiwa katika moja ya eneo ambalo watalitumia katika filamu hiyo
Akiongea na thesuperstaratz Msanii huyo mkubwa na mwenye ndoto nyingi za kukuza kiswahili barani ulaya amesema yupo nchini Uswizi kwa ajili kusoma tamaduni  za nchi hiyo ikiwa ni matayarisho ya filamu yake mpya ambayo hakuwa tayari kutaja jina lake kwa madai ya kuwa ni mapema sana,,Nipo hapa Genneva Uswizi Nkitokea denmark ambapo ndio naishi na lengo la kuja hapa ni kuangalia mazingira husika na tamaduni za Waswizi ili nitakapocheza filamu hiyo isinipe shida maana nitakuwa nime copy kila kitu cha waswizi. Alisema Selembe Ambaye kwa sasa ni lulu ya maproduser wa filamu huko barani ulaya.
Pia selembe amesema anafurahi sana kwani alipofika katika nchi hiyo tofaut na alivyokuwa anadhani amekutana na mashabiki wake wengi waliokuwa wanamuangalia tu kwenye filamu zake hivyo kupata moyo kuwa kazi anayofanya inafika kwa mashabiki zake na wanaipokea vizuri,,Kiukweli kwangu ni kama siamini kwani kitendo cha mimi kufika Uswizi na kukuta nina mashabiki wengi sana yaani nimefarijika na nina waahidi mashabiki zangu duniani kote kuwa nitafanya kazi nzuri na bora zaidi alimaliza msanii huyo wa kimataifa anayetesa na filamu za kiswahili,kiswidesh, kifaransa na za kingereza.
Thesuperstarstz inakutakia kila la kheri katika ndoto zako na kukushukuru sana kwa kuendelea kukitangaza kiswahili duniani kote

Kwa habari za wasanii africa na dunian kote tembelea hapa             www.thesuperstarstz.blogspot.com

No comments:

Post a Comment