Wednesday, November 19, 2014

KIFO CHA SEKI FAMILIA YA TOA TARIFAA KAMILI NA KUKANUSHA ZINAZOSAMBAA MITANDAONI

secky 2
Mitandao ya kijamii kuanzia kwenye Whatsapp mpaka twitter, Facebook na Instagram siku hizi imekua na nguvu kubwa na ndio maana hata taarifa zinaenea kwa kiasi kikubwa sana siku hizi bila kungoja Magazeti, Radio au TV.
Najua kama unafatilia habari zinazoendelea mjini utakua umekutana na voicenote au taarifa ya kifo cha huyu ndugu yetu inaweza kuwa imekufikia lakini sio kwa usahihi, au chanzo cha kifo kinaweza kuwa kimepotoshwa.
Sasa familia ya Marehemu Lusekelo Samson Mwandenga (Secky) imekanusha taarifa zinazoendelea kusambazwa kupitia voice note na kwenye mitandao kuhusu chanzo cha kifo chake na kwamba alikwenda kwenye birthday, ukweli ni kwamba aliumizwa na kiti cha kioo akiwa kambeba mtoto wake nyumbani kwake, akapelekwa hospitali na baadae akafariki akiwa Hospitali, hakuna kingine zaidi ya hapo.
Secky 
Secky alikua rafiki wa watu wote wakiwemo wasanii wengi wa bongofleva na hata bongomovie pia ndio maana msiba huu umewagusa kutokana na ukarimu wake kwao akiwemo Wema Sepetu ambae amesema >>> ‘Ulikua mtu wa watu, sanaaaaa…… najua utaliliwa na wengi…. they say vizuri havidumu, pumzika kwa amani baba…. It’s jus too hard to sink in….
Diamond Platnumz ameandika ‘Gone too soon my Brother… i still don’t wanna believe that you are realy Gone….dah si jana tu tumezungumza’
R.I.P Secky.

No comments:

Post a Comment