Tuesday, April 07, 2015

DIAMOND AWEKA WAZI KUHUSU YEYE KUMUOWA ZARI

Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ katika pozi.
Musa Mateja
Kutafuta kiki? Wikiendi iliyopita, gumzo kubwa katika mitandao ya kijamii lilikuwa ni kuhusu stori ya staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kufunga ndoa na mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ lakini Ijumaa Wikiendalimezungumza na mwanamuziki huyo na kupata ukweli wake.
Taarifa hizo ziliibuka katika mtandao wa Instagram mara baada ya Diamond kuweka picha iliyomuonesha akiwa na Zari ambaye alivaa shela huku Diamond akiwa na suti kuashiria kuwa wawili hao wamefunga ndoa kutokana na ujumbe uliosindikiza picha hiyo.

Diamond aliandika: “Wakati mwingine usiri una baraka zaidi...alhamdullah (sometimes privacy has more blessings...thank you so much God).”
Baada ya ujumbe huo ndipo mashabiki wao walipoanza kusambaziana ujumbe kuwa Diamond amemuoa Zari.
Baada ya kuenea kwa ubuyu huo, mwanahabari wetu alimvutia waya Diamond na kumtaka aeleze ukweli wa habari hiyo ambapo alifunguka.
Ijumaa Wikienda: Ebwana vipi hii ishu ya ndoa ni kweli umeoa?
Diamond: Suala la ndoa lipo tu kwani wewe hujui mtoto Zari ana familia yangu? Nikikamilisha mchakato naweka wazi kila kitu.
Ijumaa Wikienda: Kwa hiyo unataka kuwaambia Watanzania kwamba umeshamuoa Zari au bado?
Diamond: Taratibu za awali nyingi tumeshakamilisha lakini zaidi kuna kitu kikubwa natarajia kukifanya pale Mlimani City (Dar) na hiki kitathibitisha ukweli wa unachokiuliza.
Ijumaa Wikienda: Umesema nisubiri sawa, hiyo Mlimani City ni tarehe ngapi?
Diamond: Usijali ni Mei Mosi, mwaka huu.
Ijumaa Wikienda: Poa, kila la kheri tutajumuika pamoja siku hiyo.
Mara kadhaa Diamond amekuwa akionesha nia ya kumuoa Zari hivyo mashabiki wengi wanaamini kuwa safari hii yupo ‘siriaz’ zaidi.

No comments:

Post a Comment